Twasikitishwa na ukamataji na utesaji wa watu Thailand: UM

5 Agosti 2014

Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa hofu na vile ambavyo wanaharakati, wasomi, waandishi wa habari na wanasiasa wanakamatwa na kutiwa mbaroni huko Thailand tangu kufanyika mapinduzi ya kijeshi mwezi mwaka huu.

Ofisi hiyo inasema tangu tarehe 22 Mei Baraza la Kitaifa la amani na Utulivu nchini humo limeitisha zaidi ya watu 700 na ingawa wengi wao waliachiliwa huru baada ya wiki moja kulingana na sheria za kijeshi, dadi isiyojulikana wamezuliwa zaidi ya siku saba na kutoruhusiwa kuwa na wakili wa kuwatetea au kuonana na jamii zao.

Msemaji wa ofisi hiyo Ravina Shamdasani amesema kitendo hicho kinaelekea kuleta uvunjifu wa haki za kibinadamu na uwezekano wa kuteswa wakiwa korokoroni, hususan baada ya kisa kimoja ya mwanafunzi- Kristuda Khunasen ambaye ni mwanaharakati aliposhikwa na kufungiwa kwa siku 24. Amesema mwanafunzi hiyo alifunikwa macho kwa siku 7, kupigwa mara kadhaa hadi akapoteza fahamu baada ya kufunikwa kwa mfuko wa plastiki kichwani.

(Sauti ya Ravina)

“ Tunahimiza serikali ya Thailand kuanzisha haraka uchunguzi huru na wa kina ili kubaini utesaji dhidi ya Kristuda Khunasen ili waliohusika na ukatili huo wafikishwe mbele ya sheria”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter