Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Omar Abdi wa Canada kuwa Naibu Mkuu wa UNICEF

Omar Abdi wakati akiwasilisha bajeti ya 2014-2017 kwa bodi kikao cha 2013. Picha© UNICEF/NYHQ2013-0531/Markisz

Ban amteua Omar Abdi wa Canada kuwa Naibu Mkuu wa UNICEF

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametangaza leo kuteuliwa kwa Omar Abdi, raia wa Canada aliyezaliwa nchini Somalia, kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF.

Bwana Abdi sasa hivi ni Msimamizi wa Ukaguzi wa Matumizi ya fedha, UNICEF. Amewahi kuhudumu kama Naibu Msimamizi na Mkurugenzi wa UNICEF ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (2006-2007), na pia kama Mwakilishi wa UNICEF katika nchi kadhaa.

Ana uzoefu mkubwa kuhusu programu za UNICEF na operesheni zake.