DPRK yakubali kuanzisha kituo kuhusu haki, OCHR yapongeza

30 Mei 2014

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHR imekaribisha hatua ya Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK ya kukubali kuanzisha kituo cha masuala ya haki za binadamu. Taarifa zaidi na John Ronoh.

Hatua hiyo ya DPRK inafutia azimio la Baraza la haki za binadamu la mwezi wa Machi mwaka huu, lililotaka ofisi hiyo kufuatilia  kwa haraka iwezekanavyo yalimo kwenye ripoti ya uchunguzi wa haki za binadamu DPRK.

Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu imesema hatua hiyo itawezesha mbinu za kutilia mkazo juhudi za haki za kibunadamu, na kuwepo kwa orodha ya nyaraka kamilifu za kuwezesha uwajibikaji na pia kuendeleza ushirikiano na wahusika wote.

Imesema jambo hili litaweka mambo yote kwa uwazi na kuonekana ipasavyo.

Tangu mwezi wa Machi, kumekuwa ma majadiliano  na nchi wanachama,  wakishirikiana na Ofisi ya Haki za Binadamu, OHCHR, ili kuwezesha kuwe na Kituo cha kusimamia na kufuatilia uamuzi ya Kamisheni ya uchunguzi wa haki za binadamu ili kutekeleza maafikiano hayo.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter