Walinda amani wa UM wazungumzia majukumu yao

UN Photos//Marco Dormino
Walinda amani wa Rwanda, wakiwa kwenye ujumbe wa Mataifa nchini Mali. @

Walinda amani wa UM wazungumzia majukumu yao

Tarehe 29 Mei wiki hii, ilikuwa ni Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani. Hapa New York, kama ilivyo desturi kila mwaka, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliweka taji la kuwaenzi walinda amani waliopoteza maisha yao kwenye eneo la kumbukumbu, akizungumzia hatari wanazokumbana nazo walinda amani kila siku, wanapotekeleza majukumu yao. Kwa mengi zaidi, ungana na Alice Kariuki, akitusimulia hadi tamati.