Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya ajali za barabarani Uganda yamulikwa

Usalama barabarani (Picha ya WHO)

Hali ya ajali za barabarani Uganda yamulikwa

Tarehe 10 mwezi Aprili mwaka 2014, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuimarisha usalama barabarani. Hatua hiyo pamoja na mambo mengine ilizingatia takwimu za vifo vitokanavyo na ajali za barabarani ambapo kwa mujibu wa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu watu 3,000 hufariki dunia kila siku duniani kutokana na ajali hizo. Je hali ikoje nchini Uganda, basi ungana na John Kibego wa radio washirika Spice FM.