Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti wa madawa ya kulevya Tanzania

Udhibiti wa madawa ya kulevya Tanzania

Mkutano wa udhibiti wa madawa ya kulevya umemalizika hivi karibuni mjiniViennaAustriaambapo wakuu wa nchi na mashirika mbalimbali walijadili mbinu za kukabiliana na utenegezaji na usambazaji wa madawa hayo haramu.

Mkutano huo umefanyika wakati Umoja wa Mataifa kupitia shirikalakekudhibitiuhalifu na madawa ya kulevya UNODC likisema kuwa utengenezaji, usafirishaji na matumizi ya madawa hayo unaendelea kusababisha hatari kubwa kwa afya za watu kila mahali ukiathiri maendeleo endelevu ya nchi na kanda mbalimbali.

Mathalani Jan Eliasson Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliwataka wajumbe kuepusha vijana na kulinda mifumo ya uchumi na sheria ambayo imelegea kutokana na mfumo wa madawa ya kulevya.

Tanzaniatayari imeanza hatua za kuokoa vijana waliotumbukia kwenye madawa na wanapatiwa uragibishi kupitia makazi maalum. Je ni yapi hayo na hali ikoje basi tuangazie Tanzania Zanzibar na mwenyeji wetu ni Juma Ayoub wa radio washirika Hits Fm.