Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO alaani vikali mauaji ya mwandishi Colombia

Mkuu wa UNESCO alaani vikali mauaji ya mwandishi Colombia

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova, amelaani vikali tukio la kuuwawa kwa mwandishi wa habari Yonni Steven Caicedo  nchini Colombia aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana hapo February 19.

Mwandishi huyo ambaye amekuwa akifanya kazi na kituo kimoja cha televisheni kama mpiga picha amekuwa akiishi maisha ya kujificha ficha kwa kipindi kirefu kufuatia vitisho alivyokuwa akivipata kuhusu usalama wa maisha yake.

Akielezea tukio hilo, Bokova ametaka wahusika wake kusaka ili kufikishwa kwenye mkono wa sheria. Amesema matukio ya namna hiyo hayawezi kuvumilika kwani yana binya uhuru wa waandishi wa habari.