Plumbly alaani mashambulio yaliyotokea huko Lebanon

19 Februari 2014

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Derek Plumbly, amelaani mashambulio mawili yaliyotokea leo kwenye kitongoji cha Bir Hassan in kilicho kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut na kusababsiha vifo na majeruhi kadhaa.

Katika taarifa yake, Bwana Plumbly ametuma rambirambi kwa familia za marehemu na kuwatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa. Licha ya shambulio hilo, mratibu huyo ameisihi serikali ya Lebanon kuendelea kuwa kitu kimoja wakati huu ambapo kutonatokea mashambulio ya kigaidi yasiyochagua na yenye lengo la kuleta mgawanyiko.

Bwana Plumbly ametaka kuungwa mkono kwa serikali mpya na taasisi za dola ikiwemo jeshi na vikosi vya usalama ili kulinda amani na utulivu wa nchi hiyo. Amesisitiza azma ya jamii ya kimataifa ya kuendelea kusaidia jitihada za Lebanon katika muktadha huo.