Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yapongeza kuanza kwa mashauriano Ukraine

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yapongeza kuanza kwa mashauriano Ukraine

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imekaribisha hatua ya kuanza kwa mashauriano kati ya pande kinzani nchini Ukraine.

Mashauriano hayo yameanza baada ya maelfu ya watu kuandamana kwenye mji mkuuKievtangu mwezi Novemba mwaka jana wakipinga kile kinachoonekana kuwa ni mpango wa serikali kukataa kujiunga na Muungano wa Ulaya.

Maandamano hayo yaliendelea hata baada ya serikali kupitisha sheria za kudhibiti shughuli za vikundi vya kiraia ikiwemo uhuru wa kujumuika, mikutano na kujieleza wiki mbili zilizopita.

Msemaji wa Ofisi hiyo ya Haki za binadamu Rupert Colville amesema pamoja na kukaribisha mashauriano hayo, ofisi hiyo inataka  yake endelevu, jumuishi na yanayozingatia viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

Halikadhalika Ofisi ya haki za binadamu imepongeza hatua ya bunge laUkraineya kufutilia mbali sheria zilizopitishwa tarehe 16 mwezi Januari zinazodhibiti shughuli za vikundi vya kiraia na kumtaka Rais waUkrainekusaini sheria mpya kuashiria kutupiliwa mbali kwa sheria ya awali.

Bwana Colville amekariri wito wa ofisi hiyo wa kutaka uchunguzi huru juu ya ripoti za utekaji nyara na mateso nchini Ukraine.