WFP imepata asilimia 14 tu ya fedha inazohitaji kwa ajili ya CAR

31 Januari 2014

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema limepokea asilimia 14 tu ya dola milioni 104 ilizoomba kwa ajili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa maana hiyo WFP inapungukiwa dola milioni 95, na imesema bila ufadhili zaidi haitoweza kuendelea kusaidia mahitahi muhimu ya kibinadamu nchini humo kwa mwezi wa Machi. Itashindwa kugawa chakula ambacho kimekuwa kikiwasaidia watu 200, 000.

Kwa mujibu wa shirikahilofedha zinahitajika ili kukusanya akiba ya chakula kabla ya msimu wa mvua kuanza na barabara kushindwa kupitika. Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA ELISABETH BYRS)

 

“ WFP inakaribisha tamko la jumuiya ya kimatiafa kutoa msaada wa dola milioni 200 kwa mahitaji ya dharura Jamhuri ya Afrika ya Kati  Januari 20 huko Brussels. Hata hivyo WFP imeanzisha juhudi zote za ndani za kukabiliana na ukosefu wa chakula mwezi Januari na Februari. Lakini fedha tulizonazo sasa hazitoshi. WFP haitaweza kutoa msaada baada ya mwezi Machi”