Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNECE kupiga jeki Azerbaijan kukabili changamoto za maji

UNECE kupiga jeki Azerbaijan kukabili changamoto za maji

Baraza la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Ulaya( UNECE) limemaliza majadiliano wataalamu muhimu juu ya mageuzi ya sera nchiniAzerbaijanna kukubaliana nama ya kulipiga jeki taifa hilo katika sekta ya maji.

Baraza hilo limeafikia kuanzisha mikakati ya kuisaidia Azerbaijan kukamilisha mkakati wa kitaifa wa kuendeleza  maji katika kipindi cha miezi michache kuanzia sasa.

Hatua hiyo inafuatia majadiliano yaliyodumu kwa muda mrefu ambayo yalihusisha pia upitiaji upya wa sheria kabla ya kupitishwa kwa mradi huo ambao utaleta mageuzi katika sekta ya maji.

Kwa miaka mingi Azerbaijan imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji hivyo kufikiwa kwa makubaliano hayo kutoa mwanga mpya wa matumaini kwa wananchi.