FAO yaonya kuhusu kuibuka tena kwa kirusi A(H7N9) China

20 Januari 2014

Shirika la Kilimo na Chakula duniani, FAO limesema kuwa tishio la kuzuka upya nchiniChinakwa virusi aina ya H7N9 vinavyosababisha homa ya mafua ndege ni kubwa na kwamba hali hiyo inajitokeza wakati taifahilolikikaribia kuanza sherehe za mwaka mpya.. Grace Kaneiya na Taarifa kamili

 (RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

FAO inasema sherehe za mwaka mpya zinaenda sanjari na matukio kadhaa ikiwemo uchinjaji kuku kwa kiwango kikubwa na hivyo shirikahilolinaonya ni vyema hatua za hadhari zikachukuliwa kuepusha mazingira yoyote yanayoweza kusababisha maambukizi ya virusi hivyo na kile kingine hatari cha H5N1.

Idadi ya watu walioambukizwa virusi  vya H7N9 viripotiwe Kaskazini na Kusini mwaChinamapema mwezi Disemba mwaka jana, imeongezeka kwa kiasi.

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO linasema kuwa hali hiyo inatarajiwa kujitokeza zaidi kwani mara nyingi msimu wa baradi virusi hivyo vinatabia ya kujiongeza.

Kwa upande mwingine FAO imeanzisha juhudi za kuzisaidia nchi zilizoko hatarini kukumbwa na tatizo hilo.