Skip to main content

Japan watahadharishwa vyakula vilivyoathirika na mionzi:WHO

Japan watahadharishwa vyakula vilivyoathirika na mionzi:WHO

Watu wa Japan wameonywa dhidi ya kula vyakula vilivyoathirika na mionzi iliyovuja kutoka kwenye mtambo wa nyuklia uliharibiwa na tetemeko la ardhi na tsunami.

Shirika la afya duniani WHO linaisaidia serikali ya Japan kuwaeleza watu kutokula mboga za majani au bidhaa zitokanazo na maziwa zinazotoka eneo lililoathirika na miozni.

Kwa mujibu wa msemaji wa WHO Gregory Hartl hizi ni hatua za tahadhari, amesema mtu akila mara kadhaa bidhaa hizo zinaweza kujikusanya mwilini na pili kuna taarifa zaidi ya aina ya mionzi na bidhaa zipi zimeathirika ambazo ni vyema zikaepukwa.

Serikali ya Japan pia inaangalia kwa makini vyakula vya baharini baada ya kukuta kiwango kikubwa cha mionzi kwenye maji ya bahari.