Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa MONUSCO alaani mashambulizi ya Mayi Mayi

Mkuu wa MONUSCO alaani mashambulizi ya Mayi Mayi

Mkuu wa vikosi vya Umoja wa Mataifa MONUSCO amelaani vikali mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Mayi Mayi walioshambulia eneo la Pinga lililoko Kaskazini mwa jimbo la Kivu.

Katika shambulizi hilo lililotokea hapo siku ya jumatatu askari wanne walipoteza maisha na raia watatu walijeruhiwa.

Akielezea kusikitishwa kwake kutokana na hali hiyo, Martin Kobler amesema kuwa kuna haja ya kuimarisha vikosi vya usalama ili kukabiliana na hali hiyo.

Amewapa pole ndugu na familia ya wale waliopoteza maisha na amehaidi kuendelea kutoa mchango wa hali na mali ili kuimarisha hali ya amani.