Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kay aitaka Puntland kudumisha utulivu baada ya kubaduilishana madaraka:

Kay aitaka Puntland kudumisha utulivu baada ya kubaduilishana madaraka:

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Nicholas Kay, Jumapili ametoa wito wa kudumika amani na kufuata sheria baada ya kukabidhiana madaraka huko Puntland kufuatia uchaguzi wa Rais uliofanyika Januari 8.

Bwana Kay amesema wabunge wa Puntland wamekuwa ni mfano wa kuigwa siku chache zilizopita kwa kuonyesha uwajibikaji, amani na uwazi katika uchaguzi. Pia amepongeza Rais anaeondoka madarakani na jukumu lake katika kukabidhi madaraka.

Bwana Kay ameongeza kuwa ametiwa moyo na uhakika aliopewa na Rais mteule wa Puntland Abdiweli Mohamed Ali Gaas kwamba atachukua hatua za haraka kushughulikia maslahi ya vikosi vya usalama vya eneohilo.

Amani na mchakato wa ujenzi wa taifa unaendelea vizuri na hivyo usitibuliwe na kundi lolote au watu binafsi ameonya bwana Kay.

Amewahakikishia watu wa Puntland kuwa Umoja wa mataifa na washirika wake ,ikiwemo IGAD na Muungano wa Ulaya wataendelea kufuatilia hali Puntland na kutoa msaada wao kwa watu na uongozi wa eneo hil panpo stahili.