Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lashutumu yanayoendelea Iraq

Baraza la usalama lashutumu yanayoendelea Iraq

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo wamekuwa na kikao kuhusu hali ilivyo nchiniIraqambapo wameshutumu ghasia za hivi karibuni kwenye maeneo ya Fallujah na Ramadi kwenye jimbo la Anbar nchini Iraq. Katika kikao kilichofanyika jioni ya leo, Rais wa baraza hilo kwa mwezi huu wa Januari balozi Zaid Ra’ad Zedi Al Hassan wa Jordan alisoma taarifa yake ikishutumu ghasia hizo ikitambua kuwa vikosi vya usalama kwenye maeneo hayo vinavyopambana kudhibiti hali hiyo.  Halikadhalika wamekuwa na wito kwa jamii nzima..

(Sauti ya Balozi Al Hassan)

 "Baraza lausalama linasihi wananchi wa Iraq wakiwemo makabilia mabali mbali, viongozi wa kijamii na vikosi vya usalama kwenye jimbo la Anmbar, kuendeleza ushirikiano wao dhidi ya ghasia na ugaidi na limesisitiza muhimu wa kuendeleza mashauriano ya kitaifa na Umoja.”

Wajumbe wameunga mkono jitihada za ujumbe wa Umoja wa Mataifa  chiniIraq, UNAMI pamoja na serikali yaIraqkwa kuendelea kukidhi mahitaji ya wananchi wake hususan yale ya kuwalinda. Wamerejelea kuwa ugaidi haukubaliki kwa misingi yoyote ile.

Naye mwakilishi wa kudumu waIraqkwenye Umoja wa Mataifa amesifu tamko la Baraza la usalama na kusema pande zote zinapaswa kushirikiana kutokomeza ugaidi.