Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitendo vya uporaji na ukiukwaji mwingine lazima ukome Sudan Kusini:UM

Vitendo vya uporaji na ukiukwaji mwingine lazima ukome Sudan Kusini:UM

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande zote kuwezesha operesheni za mpango wa Umoja wa mataifa Sudan Kusini  UNMISS na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu .

Ombi hilo linajumuisha kuheshimu majengo na vituo vya Umoja wa mataifa, vifaa namalizao, kuheshimu shughuli za misaada ya kibinadamu , wafanyakazi namaliwakati wote.

Umoja wa Mataifa umeongeza kuwa wafanyakazi wasio wa serikali pia wanawajibika kisheria kuwezesha na kuheshimu operesheni za Umoja wa mataifa , wafanyakazi wa ndani na wakimataifa pamoja na mali zao.

Ilikuweza kukabiliana na changamoto kubwa zilizosababishwa na machafuko Sudan Kusini Umoja wa Mataifa unaimarisha mpango wake wa ulinzi wa amani na kuongeza misaada ya kibinadamu. Na umesema ili uweze kusaidia kulinda raia na watu wanaohitaji msaada , kupewa fursa ni muhimu saan