Ban azungumza na Rais Kiir wa Sudan Kusini

30 Disemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ambapo amesifu hatua ya kiongozi huyo ya kuazimia kusitisha chuki na utayari wa kushirikiana na wapinzani katika mazungumzo pamoja na kuwaachia mapema iwezekanavyo wafungwa wa kisiasa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema wakati wa mazungumzo hayo, Katibu Mkuu amesisitiza uungaji mkono wa Umoja huo kwa mchakato wa maridhiano ulioanzishwa na mamlaka ya IGAD na kutaka pande zote kwenye mzozo nchini Sudan Kusini kushiriki kikamilifu. Halikadhalika Bwana Ban amerejelea suala la kuwawajibisha wale wote wanaohusika na mashambulio dhidi ya raia. Viongozi hao wawili pia wamezungumzia mipango ya kuimarisha haraka iwezekanavyo kikosi cha Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS kwa mujibu wa azimio la baraza la usalama namba 2132 la tarehe 24 mwezi huu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud