UNICEF na wadau waokoa maisha ya wakimbizi watoto huko Chad

30 Disemba 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaendelea na usaidizi wake kwa raia waliokimbilia Chad kutokana na machafuko yanyoendelea huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na jimbo la Darfur nchini Sudan.  Taarifa zaidi na Grace Kaneiya

(Taarifa ya Grace)

Wakimbizi hao ni pamoja na watoto ambao wanakosa hakiyaoya msingi ya elimu pamoja na kuwa na msongo kutokana na yale waliyoshuhudia. Mshauri nasaha kutoka shirika la kiraia linalosaidiana na UNICEF kuokoa watoto Hassan Saleh Hassan anasema..

 (Sauti ya Hassan)

"Mara kwa mara tunawauliza watoto kuhusu uzoefu wao. wanasema wameshuhudia miili ya watu iliyotelekezwa barabarani na mingine kwenye mashimo. Michezo tunayowapatia inawasaidia kusahau yale waliyoyaona.”

Ili kufanikisha mustakhbali wa watoto, UNICEF na wadau wake wanaimarisha usaidizi kama anavyosema Bruno Maes, mwakilishi mkazi wa shirika hilo nchini CHAD.

 (Sauti ya Bruno)

"Wadau wote ikwemo UNICEF wanahakikisha hatua sahihi zinachukuliwa kusaidia watoto ambao ni sehemu ya wakimbizi wanaoingia Chad kutoka Jamhuri ya AFrika ya Kati na Darfur. Hiyo ni kuhakikisha haki zao za kuishi na elimu zinashughulikiwa kwa njia sahihi.”

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter