Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua makamu wa rais wa zamani Ecuador kuwa mwakilishi wake kwa watu wenye ulemavu

Ban amteua makamu wa rais wa zamani Ecuador kuwa mwakilishi wake kwa watu wenye ulemavu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua aliyekuwa makamu wa rais wa Ecuador Lenín Voltaire Moreno Garces kuwa mwakilishi wake kwa ajili ya watu wenye ulemavu na wale wanaokosa fursa.

Katika wadhifa wake huo mpya,Bwana.Morenoatachukua jukumu la kuhakikisha kwamba haki za watu wenye ulemavu zinazingatiwa. Inakadiriwa kwamba watu wenye ulemavu duniani wanafikia zaidi ya milioni moja.

Kwa hivi sasa Bwana Moreno ni mwenyekiti wa kamati ya kutokomeza aina yoyote ya unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu.