Mkuu wa UNAMID akaribisha hatua ya SLA/Minni Minawi ya kupiga marufuku kuingizwa watoto jeshini.

18 Disemba 2013

Mjumbe  maalum wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Mohamed Ibn Chambas amekaribisha hatua iliyochukuliwa na kundi la Sudan Liberation Army/Minni Minawi la kusitisha matumizi ya watoto kama wanajeshi. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(Ripoti ya Jason)

 Bwana Chambas amesema kuwa UNAMID imekaribisha hatua ya kundi la SLA/MM ya kuheshimu sheria za kimataifa  za kulinda watoto dhidi ya vitendo vya ghasia akiongeza kuwa kuwatumia watoto kwenye jeshi ni uhalifu mkubwa ambao sio tu unahatarisha maisha yao bali pia unaathiri maisha yao ya baadaye.

Amri ya kusitisha kuingizwa kwa watoto jeshini  iliyotolewa na kamanda wa SLA Minni Minawi inajiri baada ya kamanda huyo kuhudhuria warsha kuhusu usalama na  amani mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kati ya tareeh 9 na 11 mwezi huu wasrsha iliyoandaliwa Kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika

Warsha hiyo ilijadili masuala kadha kuhusu sheria ya kibinadamu ya kimataifa na haki za binadamu.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter