Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yasihi vikundi vyenye silaha kuzisalimisha

MONUSCO yasihi vikundi vyenye silaha kuzisalimisha

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO umerejelea wito wa kuvitaka vikundi vyenye silaha nchini humo kusalimisha silaha hizo kwa ujumbe huo.

Akizumgumza  katika mkutano wa waandishi wa habari na kunukuliwa  radio washirika Okapi mkuu wa MONUSCO wilayani Ituri, M’hand  Ladjouzi amesema ofisi hiyo kwa kushirikiana na serikali ya DRC iko mbioni kuanzisha tena mpango wa kuwapokea wenye silaha na kuonya kuwa kama vikundi hivyo havitaikitikia wito huo vitapokonywa silaha.

(Sauti Ladjzouzi)