Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji 100,000 raia wa Ehiopia warejea nyumbani kutoka nchini Saudi Arabia

Wahamiaji 100,000 raia wa Ehiopia warejea nyumbani kutoka nchini Saudi Arabia

Idadi ya wahamiaji raia wa Ethiopia wanaorejea nyumbani kutoka nchini Saudi Arabia imepita watu 100,000 kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Jason Nyakundi na maelezo kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

IOM inasema kuwa shughuli ya kurejea nyumbani kwa wahamiaji hao ina gharama kubwa na inatoa ombi la dola milioni 13 za kuwasaidia wahamia ambao wengi wamerudi nyumani mikono mitupu.

Idadi ya ndege zilizokodihswa kuwarejesha nyumbani wahamiaji hao zimeongezeka kutoka safari sita kwa siku hadi safari 20 . Wengi wa wale wanaowasili ni wanaume lakini pia kuna watoto wasio na wazazi.

Mara wanapowasili wahamiaji hao huandikishwa na kupewa chakula na dola hamsini za kuwazesha kusafiri kwenda makwao.

Sharon Dimanche kutoka IOM mjiniAddis Ababaanasema kuwa  wengi wa wahamiaji ni waathiriwa w biashara haramu ya watu  lakini pia ni miongoni mwa wale haki zao zimekiukwa nchiniSaudi Arabia.

 (SAUTI YA SHARON DIMANCHE)

“Hadi jana wahamiaji 100,620 wamerejea. IOM imetoa misaada kwa zaidi ya watu 90,000 miongoni mwa wahamiaji hawa. Idadi inazidi kupanda na kwa sasa tunaandikisha wahamiaji 7000 kila siku.

Yale wanayotuambia yanahusu ubakaji na dhuluma. Wanaume wameshuhudia wake zao wakibakwa. Wanawake wahahisi kuchafuliwa baaada ya vitendo hivyo.

Kundi la kwanza kuwasili pia lilisema kuwa walipigwa na kundi ya vijana kwenye mitaa ya Saudi Arabia  na wengi  hawakuwa wamelipwa mishahara yao hadi wakati walipokuwa wakiondoka kuelekea Ethiopia.

Walipokonywa pesa zao, viatu , wengi wakiwasili na nguo zilizoraruka, wachafu na bila viatu. Wanatala kutafuta fursa nzuri kwingine na sio  sisi tu kama IOM bali washirika wengine tunahitaji kushughulikia hili  kubaini ni kwa nini watu hawa wakaondoka nchini Ethiopia.”

Maelfu ya wahamiaji wengine raia wa Yemen Ethiopia wamezuliwa na wanarudishwa kwenda nchi zao .