Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano toka jumuiya ya kimataifa ndio unaochagiza mafanikio:Kaag

Ushirikiano toka jumuiya ya kimataifa ndio unaochagiza mafanikio:Kaag

Ushirikiano kutoka jumuiya ya kimataifa ni muhimu katika kufanikisha mchakato wa uchunguzi wa silaha za kemikali nchini Syria amesema mratibu maalum wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na OPCW Sigrid Kaag katika mahojiano maalum na idhaa ya kingereza ya Umoja wa Mataifa.

Bi Kaag amesema ushirikiano toka nchi wanachama wa makataba wa uteketezaji wa silaha za kemikali katika sekta mbalimbali ikiwamo fedha na mafunzo huchagiza mafanikio hayo.

(SAUTI YA KAAG)

"Tangu siku ya kwanza kumekuwa na ushirikiano mkuu toka kwa jumuiya ya kimataifa. Nchi nyingi zimekuwa zikitoa misaada kupitia vifaa, mafunzo, usafiri mathalani Marekani imekuwa ikitoa msaada katika kuhakikisha tunafanikisha ikiwamo msaada muhimu wa fedha kwa OPCW Na Umoja wa Mataifa ."