Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UNAMID apongeza amani Mashariki mwa Darfur

Mjumbe wa UNAMID apongeza amani Mashariki mwa Darfur

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mzozo wa Darfur nchini Sudan Mohamed Ibn Chambas amekamilisha ziara yake ya siku mbiuli kutembelea eneo la El Daein lililoko Mashariki mwa Darfur na kupongeza mamlaka kwenye eneo hilo kwa kuimarisha amani.

Mjumbe huyo amewapongeza viongozi wa jadi ambao amesema kuwa wamejifanikiwa kuleta upatanishi na kumaliza mapigano yaliyoibuka Agosti mwaka huu baina ya watu wa Rezeigat na  Ma’aliya

Mwanadiplomasia huyo amesema kuwa UNAMID itaendelea kushirikiana na pande zote ili kuhakikisha kwamba agenda ya amani na usalama inakuwa ya kudumu na kukubaliuwa na kila pande.

Aliwataka wakazi wa eneohilokutambua kwamba mtutu wa bunduki hauwezi kamwe kuleta amani bali kwa majadiliano ya amani amani ya kudumu inaweza kupatikana.

Katika ziara yake hiyo mwanadiploamsia huyo alikutana na kuzungumza na viongozi mbalimbali kiwemo wale wa kikoo