Burundi yakabiliwa na changamoto ikijiandaa na uchaguzi wa 2015:

2 Disemba 2013

Mchakato wa kuelekea uchuguzi mkuu wa Burundi hapo 2015 uliopitishwa mapema mwaka huu umetathiminiwa wiki hii na vyama vya siasa vya Burundi na wadau wengine kwenye mkutano wa siku tatu ulioandaliwa na serikali yaBurundi na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo BNUB.

Mkutano huo ulioanza Novemba 27 na kukamilika Novemba 29 umetathimini utekelezaji wa mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu na kunabhisha changamoto na fursa zilizopo kwa ajili ya kuimarisha majadiliano na utamaduni wa demokrasiaBurundi. Mkuu wa BNUB na mwakilishi wa Katibu Mkuu nchiniBurundini Parfait Onanga-Anyanga

 (SAUTI YA PARFAIT ONANGA-ANYANGA)

"Wote walikubaliana kwamba kuna haja ya utashi wa kisiasa nhcini na kukubaliana kwamba misukosuko bado ni mingi na mazingira sio mazuri kwa uchaguzi ujao. Pia wadau walitambua kwamba kutovumiliana na ghasia za kisiasa bado ni changamoto nchini kwa sababu inahusisha hasa kundi muhimu la jamii ambao ni vijana. Kwa sasa wanajaribu kutatua swala hilo ambalo kwa mamlaka za Burundi zinataka kukabiliana na changamoto hiyo kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015"

Mchakato huo ulipitishwa mwisho mwa warsha iliyofanyika Machi 2013 baada ya kubaini somo walilojifunza baada ya uchaguzi mkuu wa 2010.

Mchakato huo umehusisha vyama na wadau wa siasa zaidi ya 40 wakiwemo wale walioondoka nchiniBurundibaada ya uchaguzi wa 2010.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter