Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maziwa na bidhaa za maziwa ni muhimu kwa lishe ya watu masikini:FAO

Maziwa na bidhaa za maziwa ni muhimu kwa lishe ya watu masikini:FAO

Shirika la mpango wa chakula duniani FAO linazitaka serikali kuhakikisha maziwa na bidhaa zake zinapatikana kwa familia za watu masikini kabisa duniani.

Kwa mujibu wa ripoti yake ya karibuni maziwa na bidhaa za maziwa sio tuu zinaweza kuboresha lishe ya watu masikini bali pia zinaweza kuinua uchumi wa familia za wafugaji na wazalishaji wa bidhaa za maziwa.

FAO inasema faida za bidhaa hizo ni kuanzia kwa watu binafsi, jamii zinazowazunguka na hatimaye kwa maendeleo ya taifa.

Ripoti hiyo inatathimini uhusiano uliopo baina ya lishe na matumizi ya bidhaa za maziwa, mapungufu na kutanabaisha athari nzuri za kuwekeza katika mipango ya uzalishaji wa maziwa na bidhaa zake. Bi Ellen Muehlhoff ni afisa wa lishe wa FAO anaeleza ni kwa nini maziwa na bidhaa za maziwa ni muhimu kwa lishe na afya

(SAUTI YA ELLEN MUEHLHOFF)