Watoto 6000 vitani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati: UNICEF

22 Novemba 2013

Kundi moja lililojihami nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limewaingiza karibu watoto 6000 kwa jeshi lao kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi.

(Taarifa ya Jason)

Karibu nusu ya watoto hao wameingizwa jeshini mwaka huu kufuatia kupinduliwa kwa serikali na waasi mwezi nMachi. UNICEF inasema kuwa hali ya usalama kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati inasalia kuwa mbaya huku makundi yaliyojihami yakiendelesha dhuluma. Raia waliojipata ndani ya mapigani wamebuni makundi yao ya kujilinda ambapo pia makabiliano kati ya wakristo na waislamu yakishuhudiwa kila siku. Mkurugenzi wa UNICEF nchini humo Souleymane Diabate hata hivyo anasema kuwa baada ya kuwepo kwa hali mbaya ya usalama UNICEF inaendela na shughuli zake za utoaji wa huduma za kibinadamu.

(Sauti ya Diabate)

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa karibu nusu ya waakazi wote milioni nne nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanahitaji huduma za kibinadamu.