Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Urejeshaji wa wakimbizi wa Burundi walioko Uganda wamulikwa

Urejeshaji wa wakimbizi wa Burundi walioko Uganda wamulikwa

Burundi,Ugandana Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR wamefikia makubaliano ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Burundi waliochukua hifadhi  nchiniUganda. Hii ni baada ya kikao cha pande hizo tatu kilichofanyika hivi karibuni mjini Bujumbura Burundi.Uganda imewapa hifadhi zaidi ya wakimbizi elfu 10 kutoka Burundi, sehemu kubwa walikimbia machafuko ya mwaka wa 1993. Shughuli hiyo ya kuwarejesha wakimbizi waBurundiwaliokoUgandaitasimamiwa na Shirika la UNHCR mwanzoni mwa mwaka ujao.

Je ni kipi kilichokubaliwa? Na mchakato utakuwa vipi? Ungana basi na mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA kutokaBujumbura.

 STUDIO: PCKG ya RAmadhani Kibuga