Nchi 14 zaungana na wenzao katika ujumbe wa Baraza la Haki za Binadamu

12 Novemba 2013

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo pamoja na majukumu mengine lilikuwa na kazi ya kuchagua wajumbe 14 wa Baraza la Haki za binadamu watakaohudumu kwa miaka mitatu kuanzia mwezi Januari mwakani.

Uchaguzi huo umefanyika ili kuziba nafasi hizo zitakazoachwa wazi pindi nchi 14 zitakapomaliza ujumbe wao mwishoni mwa mwaka huu. Rais wa Baraza Kuu John Ashe alitangaza taratibu za kupiga kura na kueleza bayana kuwa kipindi cha ujumbe ambacho kinamazika Juni sasa kinamalizika mwezi Disemba.

Nchi 28 zilijitokeza kuwania nafasi hizo zilizokuwa zimeganywa kwa makundi ambapo bara la Afrika nafasi Nne, Asia na Pasifiki Nne, Ulaya Mashariki mbili, Amerika kusini na Karibeani Mbili halikadhalika nafasi mbili kwa Ulaya Magharibi na mataifa mengine. Bwana Ashe akatangaza nchi zilizoibuka kidedea.

(Sauti ya Ashe)

Baraza la haki za binadamu lina wajumbe 47.