Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR Kutumia ndege kusaidia waathirika wa kimbunga Typhon nchini Ufilipino

UNHCR Kutumia ndege kusaidia waathirika wa kimbunga Typhon nchini Ufilipino

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetangaza leo kwamba linatoa msaada wa huduma za dharura kwa kutumia ndege nchini Ufilipino ambapo inakadiriwa watu milioni 9.8 wamethiriwa na kimbunga Typhhon kilichoikumba nchi hiyo wiki iliyopita.

Taarifa ya shirika hilo imemkariri Kamishana Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres akisema ingawa shirika lake hufanya kazi zihusuzo mafarakano lakini janga hili linahitaji kila juhudi ziwezekanazo katika ili kusaidia watu walioathirika.

UNHCR tayari imeshatoa msaada wa katika eneo la Cotabato, Mindanao na linatuma huko Tacloban vifaa vya ulinzi 1, 400 na vifaa vya usafi vinavyojumuisha vitu vya msingi kama vile mablangeti, mashuka, vyandarua, sabuni na nguo za ndani.

Taarifa hiyo inasema ili kukamilisha msaada huo wa dharura UNHCR imeandaa doala milioni tatu zitokanazo na hifadhi ya operesheni zake mjini Genevana kaisi cha dola milioni 10 kitatafutwa ili kutoa misaada na kuokaoa maisha kwa miezi mitatu.