Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mimba za utotoni zaangaziwa Tanzania

Mimba za utotoni zaangaziwa Tanzania

Mapema wiki hii shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA lilitoa ripoti yake kuhusu idadi ya watu ikiangazia zaidi mimba za utotoni. La kustaajabisha ni kwamba takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka, watoto milioni 7.3 wa kike chini ya umri wa miaka 18 hupata ujauzito na kwamba Milioni Mbili katiyaowana umri usozidi miaka 14. Nchini Tanzania hali ikoje? Tamimu Adam na Enesi Mwaisakila wa Radio Washirika ya Jogoo FM huko Ruvuma Tanzania wanaangazia hali ilivyo katika makala hii ya wiki tafadhali ungana nao.

( PCKG ya TAMIMU ADAM na ENESI MWAISAKILA)