Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nuru yaonekana kuelekea mkutano wa pili wa Geneva kuhusu Syria: Brahimi

Nuru yaonekana kuelekea mkutano wa pili wa Geneva kuhusu Syria: Brahimi

Nchini Syria matumaini ya kupatia suluhu ya amani mzozo unaoendelea yanaanza kuonekana kufuatia ziara ya mjumbe wa pamoja wa Umoja wa mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi kwenye ukanda huo. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Ripoti ya Assumpta)

Ziara ya Brahimi huko Mashariki ya Kati ilianza mwishoni mwa wiki ambapo nchi alizopita ni pamoja na Misri, Iran, Oman na Syria ambapo amesema kote huko wameonyesha matumaini yao kwa mkutano wa Geneva kutokana na adha ya janga linaloendela na machungu wanayopata raia wa Syria nyumbani na ugenini. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Damascus amesema pande zote Syria zina hofu juu ya hali ya nchi yao na wanataka kuona suluhu inapatikana hususan kupitia mkutano wa Geneva ambao unatekeleza makubaliano ya tarehe 30 Juni 2012.

(Sauti ya Brahimi)

Katika hatua nyingine shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema limekamiilsha mgao wa chakula kwa mwezi Oktoba uliofikia wasyria Milioni Tatu nukta Tatu na kuwa ni mgao mkubwa zaidi nchini humo tangu mwaka 2011. Hata hivyo WFP imesema idadi hiyo ni pungufu ya lengo lao la awali la kufikia watu Milioni Nne kutokana na hali mbaya ya usalama huko Aleppo na Hassekeh.