Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

M23 wajisalimisha, mji wa Bunagana sasa chini ya FARDC: MONUSCO

M23 wajisalimisha, mji wa Bunagana sasa chini ya FARDC: MONUSCO

Mnamo mwezi Oktoba, idadi kubwa ya wapiganaji wa kundi la waasi la M23 walijisalimisha kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kuweka Utulivu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, MONUSCO. Hapo jana tarehe 29 Oktoba, wapiganaji wengine 33 wa M23 walijisalimisha, na hivyo kupelekea idadi ya wapiganaji wa M23 walojisalimisha kwa MONUSCO kufika 80 katika mwezi wa Oktoba pekee.

Katika Kivu ya Kaskazini, MONUSCO imesema mamia ya wakimbizi wa ndani katika eneo la Kanyaruchinya wanaondoka na kurejea Kibumba, yapata kilomita 27 kaskazini mwa Goma, ambako walitoka kufuatia mapigano ya wiki ilopita.

MONUSCO imesema inafanya doria za mara kwa mara kutoka Kanyaruchinya hadi Kibumba ili kuhakikisha usalama wa raia.