Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani shambulizi liliouwa makumi ya raia Afghanistan

UNAMA yalaani shambulizi liliouwa makumi ya raia Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani shambulio lililofanywa jana jimboni Ghazni ambapo kifaa kilicholipuka kilisababisha vifo vya watu 19 na majeruhi waliokuwa wakisafiri katika bus dogo ambapo waliouwawa ni pamoja na wanawake 16 na watoto kadhaa.

Grace Kaneiya na taarifa kamili

Mkuu wa UNAMA Ján Kubiš amesema tukio la jana ni mfululizo wa milipuko inayosababisha vifo vya raia wa nchi hiyo na kutaka kukomeshwa kwa mashmbulio hayo hima.

Takwimu zilizotolewa na UNAMA zinaonyesha kuwa mashambulio kama hayo ndiyo yanayoongoza kwa kuuwa na kujeruhi raia nchini Afghanstan nchi ambayo inashuhudia mapigano ya vikundi vyenye silaha. Mathalani kuanzia mwezi January hadi October mwaka huu watu 828 samekufa na 1627 kujeruhiwa . Idadi ya majeruhi kutokana na milipuko ya vifaa mbalimbali imeongezeka kwa asilimia 13 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana huku pia majeruhi wakiongezeka kwa ailimia 17 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka 2011.

Licha ya kutoa salamu za rambirambi na kuwatakiwa majeruhi uponyaji wa haraka UNAMA imeonya kwamba matumizi ya vifaa vya milipuko ya kiholelea yataongeza uhalifu wa kivita nchini Afghanstan.