Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visasi dhidi ya wanaharakati China vyatia hofu: Wataalamu

Visasi dhidi ya wanaharakati China vyatia hofu: Wataalamu

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu limeelezea masikitiko yake kutokana na ripoti zinazoeleza kuwa watetezi wa haki za binadamu nchini China wanaandamwa na vikwazo vya kushiriki kwenye tukio muhimu la kutathmini mwenendo wa taifahilokuhusiana na haki za binadamu. George Njogopa na taarifa kamili

 (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 Ripoti zinasema kwamba wanaharakati hao wa kutetea haki za binadamu wamekuwa wakiandamwa na matukio mbalimbali ikiwemo yale ya kutishiwa kutiwa korokoroni na kupigwa marafuku kushiriki kwenye mikusanyiko yoyote. Pia wamezuiliwa kutoondoka nchini humo ama kwenda kushiriki kwenye kongamano lililoandaliwa na Baraza la haki za binadamu linalotazamiwa kukutana baadaye mwaka huu kuijadili mwenendo waChinakuhusiana na haki za binadamu.  

Baraza hilo kila baada ya kipindi fulani hukutana na kutathmini hali ya haki za binadamu kwa nchi iliyopendekezwa.Mwaka huu baraza hili linatazamiwa kukutana Oktoba 22 huko Geneva. Mmoja wa wataalamu wa haki za binadamu Maina Kiai amesema kuwa kuwapiga marafuku watu kushiriki kwenye kikao hicho kijacho ni kuvunja wajibu wa kimataifa ambao China inapaswa kuuzingatia.