Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali kwa watetezi wa haki za binadamu nchini Togo imeboreka: Sekaggya

Hali kwa watetezi wa haki za binadamu nchini Togo imeboreka: Sekaggya

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu Margaret Sekaggya ametoa wito kwa serikali ya Togo kuhakikisha kuwa watetesi wa haki za binadamu wana mazingira bora ya kufanya kazi  bila  kukandamizwa au kushutumiwa. Bi Sekaggya amesema kuwa hali kwa waetesi wa haki za binadamu na mashirika ya umma nchini Togo imeimarika ikilinganishwa na kile alichoshohudia mwaka 2008 ambapo amepongeza utawala , mashirika ya umma na jamii ya kimataifa kwa jitahada zao.

Mjumbe huyo amesema kuwa uandishi wa habari nchini Togo ambao ni mchanga haufanyiki kwa viwango vinavyohitajika . Bi Sekaggya ameelezea wasi wasi wake kufuatia matumizi ya nguvu kutoka kwa polisi wakati wakikabiliana na maandamano akiongeza kuwa maafisa wa usalama wanastahili kupewa mafunzo jinnsi  ya kukabilina na watu wengi..