Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauaji ya walinda amani watatu wa UNAMID

Ban alaani mauaji ya walinda amani watatu wa UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la Jumatatu lililofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya msafara wa mpango wa pamoja wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika Darfur UNAMID.

Shambuliohilolimekatili maisha ya walinda amani watatu na kujeruhi mmoja, wote wakliwa ni raia waSenegal. Ban ametoa salamu za rambirambi kwa familia na jamaa ya waliopoteza maisha , ikiwa ni pamoja na kwa serikali yaSenegal.

Ban amesema mara nyingi walinda amani wa UNAMID wanashambuliwa na kupoteza maisha wakiwa kazini, wakati wanawasaidia Wasudan kurejesha amaniDarfur. Amesema mashambulizi hayo hayakubaliki na ameitaka serikali ya Sudankuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria.