Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha mkutano wa kumaliza migogoro Myanmar

UM wakaribisha mkutano wa kumaliza migogoro Myanmar

Umoja wa Mataifa umekaribisha maamuzi ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa makabila yote yenye silaha nchini Myanmar ili kuungana, mkutano ambao unaimarisha tumaini la kumalizika kwa amani kufuatia vita vilivyodumu kwa zaidi ya nusu karne nchini humo na kuanza kwa majadiliano ya kisiasa.

Hayo yamebainishwa katika taarifa ya mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Myanmar Vijay Nambiar ambaye alihudhuria akiwa ni mwangalizi katika mazungumzo ya amani kati ya serikali ya nchi hiyo na taasisi iitwayo Kachin Independence (KIO)

Bwana Nambiar amesema uwakilishi wa vyama vya kisiasa na asasi za kiraia ulitambulika na kuelezea matumaini yake ya kuimarika kwa hali nchini humo na kusisitiza uwakilishi wa ngazi zote na pande zote ili kutafuta suluhu kwa njia ya majadiliano. Amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia na kuunga mkono watu wa Myanmar wakati huu ambapo nchi inaendelea katika mchakato wa kuelekea amani na demokrasia.