Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay akaribisha ripoti ya uchunguzi Sri Lanka

Pillay akaribisha ripoti ya uchunguzi Sri Lanka

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekaribisha kutolewa kwa ripoti iliyoangazia machafuko ya Sri Lanka na ameunga mkono mwito uliotolewa na ripoti hiyo ambayo imetaka kufanyika kwa uchunguzi zaidi wa kimataifa.

Akijadilia ripoti hiyo ambayo imetolewa na jopo la wataalamu, Bi Pillay amesema kuwa pamoja na kwamba taarifa zilizopo kwenye ripoti hiyo zinaweza kuwashtua wengi na kuleta huzuni lakini bado inatoa sura ya kile kinachopaswa kuchukuliwa sasa.

 

Amesema kama ripoti ilivyobainishwa kuwa suala la kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinalindwa na kuzingatiwa kwa sheria za kimataifa kuwa siyo suala la hiari wala la kisera bali lazima kutambua kwamba wahusika wake wanapitiwa na mkono wa sheria.

 

Aidha ameitaka serikali ya  Sri Lanka kuchukua hatua za haraka kama ilivyopendekezwa na wataalamu hao ili hatimaye kuwatendea haki waathirika wa matukio ya vita.