Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuitembelea India

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuitembelea India

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Christof Heyns anatarajiwa kuizuru India kuanzia tarehe 19 hadi 30 mwezi huu ziara ambayo itakuwa ya kwanza kufanywa nchini humo na mtaalamu huru aliyetumwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza mauaji ya kikatili nchini humo.

Heyns anasema kuwa ziara hii itampa fursa nzuri ya kuchunguza mauaji ya kikatili nchini India na jitihada zinazofanywa katika kuzuia mauaji hayo. Mjumbe huyo atatoa mapendekezo ya kuisaidia nchi hiyo katika kulinda maisha ya binadamu . Kwenye ziara ambayo itamchukua siku 12 mtaalamu huyo atautembelea mji wa New Delhi na majimbo kadha ambapo atakutana maafisa wa ngazi za juu pamoja na wasomi kadha yakiwemo pia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na yale ya Umoja wa Mataifa.