Kikao cha kwanza cha mawaziri wa Afrika kuhusu Tabianchi kufanyika Arusha

9 Oktoba 2013

Huko Arusha, Tanzania kikao cha kwanza cha aina yake kuhusu mabadiliko ya tabianchi kikihusisha mawaziri na wadau wa sekta hiyo kutoka barani Afrika kinaanza Alhamisi. Lengo ni kuibuka na mikakati mipya kuhusu mfumo wa tabianchi barani Afrika na kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa kama anavyoripoti George Njogopa.

(Taarifa ya George Njogopa)

Mkutano huo unaojulikana pia kama AMCOMET unatazamiwa kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na baadaye kufuatiwa na hotuba itakayowsilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa shirika la hali ya hewa duniani Jerry Lengoasa. Lengosa atazungumzia mada iliyopewa jina la “ ufahamu agenda za utafiti wa hali ya hewa kwa Afrika”mada ambayo imeandaliwa mahasusi kwa ajili ya kupunguza pengo la uhaba wa taarifa za utafiti kwa nchi za afrika AMCOMET ,ni jitihada za pamoja baina ya Shirika la hali ya hewa duniani na Umoja wa Afrika kwa shabaha ya kuleta uelewa wa hali ya hewa na vipaumbele vyake. Mkutano huo utamulika zaidi eneo la utafiti na maarifa.