Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikundi 130 kutoka Afrika vyataka ICC iungwe mkono

Vikundi 130 kutoka Afrika vyataka ICC iungwe mkono

Huko Johannesburg, Afrika Kusini vikundi 130 barani Afrika vimeweka hadharani baruayaoinayotaka nchi za barahilozilizo wanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC kuunga mkono mahakama hiyo wakati wa kikao maalum cha wakuu wa nchi za Muungano wa Afrika. Kikao hicho kitafanyika tarehe 11 na 12 mwezi huu hukoAddis Ababa. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Vikundi hivyo kutoka nchi 34 za Afrika vimesema Afrika ni lazima iunge mkono mahakama ya ICC ikiwemo kesi zinazoendelea kuhusu uhalifu uliotendwa nchiniKenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Uhusiano kati ya ICC na mataifa kadha ya bara la Afrika umekumbwa na changamoto wakati kesi hizo zikendelea.

Hali hii imesababisha kuibuka madai kuwa ICC inalenga tu mataifa ya Afrika huku kukiibuka maswali mengi iwapo mataifa ya Afrika yaliyo wanachama wa ICC yatajiondoa kwenye makubaliano ya Roma yaliyobuni mahakama hiyo. Kusini mwa Afrika taifa laBotswana limekuwa muungaji mkono mkubwa wa mahakama ya ICC wakati ambapo mataifa mengine ya Afrika yakisalia kimya. Mataifa ya Afrika yalichukua nafasi kubwa kwa mazungumzo yaliyochangia kuanzishwa ICC.