Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaunga mkono hatua ya Jumuiya ya Ulaya kuhusu matumzi ya tumbaku

WHO yaunga mkono hatua ya Jumuiya ya Ulaya kuhusu matumzi ya tumbaku

Ikiwa imepita zaidi ya miaka kumi tangu kutekelezwa kwa mkataba wa Jumuiya ya Ulaya kuhusu matumizi ya tumbaku mwaka 2001, Jumuiya ya Ulaya imekuwa kwenye mstari wa mbele katika  kupunguza matumizi ya bidhaa  hizo.

Kila mwaka matumizi ya tumbaku na pamoja na madhara ya moshi vimechangia vifo vya zaidi ya watu 700,000 barani ulaya.Kama mwanachama wa mkataba huo Jumuiya ya ulaya ina jukumu la  kuimarisha sheria zinazosimamia matumizi ya tumbaku kuambatana na viwango vya kimtaiafa. Wanachama kwenye makubaliano hayo wanatakiwa kuchukua hatua kadha kupunguza uzalishaji na matumizi ya bidhaa za tumbaku na kuwakinga watu wanoathiriwa  na moshi utokanao na tumbaku, kupiga marufuku matangazo ya bidhaa za tumbaku, ufadhili, kuzuiwa kuuzwa kwa bidhaa hizo kwa watoto na kuweka onyo la kiafya kwa pakiti za bidhaa za tumbaku.

Mkataba huo wa Jumuiya ya Ulaya hautaokoa maisha tu na kukinga vijana kuwa na uraibu wa kutumia bidhaa za tumbaku bali pia utatoa ishara kwa ulimwemgu kuwa Jumuiya ya ulaya inaendelea kuwa muungaji mkono mkubwa kwenye vita dhidi ya matumizi ya tumbaku.