Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Babacar Cissé wa Senegal kuwa naibu mwakilishi wake maalum Côte d’Ivoire

Ban amteua Babacar Cissé wa Senegal kuwa naibu mwakilishi wake maalum Côte d’Ivoire

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bwana M’Baye Babacar Cissé wa Senegal kuwa naibu mwakilishi wake maalum wa Operesheni za Umoja wa Mataifa nchini Côte d’Ivoire, UNOCI, ambako pia atahudumu kama Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa, Mratibu wa Maswala ya Kibinadamu na Mwakilishi Mkaazi wa UNDP.

Bwana Cissé atachukuwa nafasi ya Ndolamb Ngokwey wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambaye Katibu Mkuu amempongeza kwa huduma yake ya kujitoa, na kwa mchango wake kwa kuboresha uratibu wa mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

Bwana Cissé ana uzoefu mkubwa katika masuala ya maendeleo na misaada ya kibinadamu barani Afrika, ikiwemo katika mikakati ya kikanda na harakati za ushrikiano wa mashirika mbali mbali. Amefanya kazi na Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1980, na hivi majuzi amekuwa makamu wa naibu msaidizi wa msimamizi na mkrugenzi wa kikanda wa Shirika la Mpango wa Maendeleo, UNDP barani Afrika.