Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Navi Pillay awalilia wahamiaji waliofariki dunia kwenye ajali ya maji Italia

Navi Pillay awalilia wahamiaji waliofariki dunia kwenye ajali ya maji Italia

Mkuu wa Kamishna ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Navi Pillay ameelezea kushtushwa kwake na taarifa za vifo vya wahamiaji wa Afrika waliofariki dunia kwa ajili ya maji wakati wakielekea nchini Italia kwa usafiri wa boti.

Pamoja na kuelezea masikitiko yake, Pillay amepongeza hatua zilizochukuliwa na serikali ya Italia ambayo ilifaulu kuwaokoa baadhi ya wahamiaji kwenye boti hiyo.

Hata hivyo ameitaka Italia na Jumuiya ya Kimaraifa hasa Umoja wa Ulaya kuhakikisha kwamba matukio kama hayo hayajirudii tena.

Amesema anaingiwa na hofu kuona vitendo vya magendo na usafirishaji watu na idadi ya wakimbizi ikiongezeka katika eneo la Mediterranean na kwingineko ikiwemo eneo Ghaba ya  Aden.