Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yaandaa mkutano wa kutatua mizozo ya kikabila jimbo la Darfur

UNAMID yaandaa mkutano wa kutatua mizozo ya kikabila jimbo la Darfur

Zaidi ya viongozi 100 wa makabila kwenye jimbo la Darfur kutoka makabila yote kaskazini mwa Darfur walikusanyika kwenye mkutano wa siku mbili kujadili janzo cha ghasia za kikabila kwenye jimbo la Darfur ambapo walipendekeza suluhu ya kuleta amani katika eneo hilo. Mkutano huo ulioandaliwa na ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika UNAMID ulifanyika mjini El Fasher na kukamilika hapo jana.

Mkuu wa masuala ya umma kwenye ujumbe ya UNAMID Retta Reddy amesema kuwa ili kutatua mzozo ulio Dafur ni lazima kuwe na usawa kwenye ugavi wa raslimali kuhakikisha kuwa kila mmoja amefaidika. Washiriki wote kwenye mkutano walitaka kuwekwa sheria zinazosimaia masuala ya ardhi na raslimali , wakataka kufanyika kwa mabadiliko mahakamani , kuwekeza kwa sekta ya mifugo na kutekelezwa kwa makubalino ya Doha.