Ban asikitishwa na kifo cha askari wa Sierra Leonne huko Sudan

1 Oktoba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amesikitishwa na kifo cha askari mshauri kutoka Sierra Leone ambaye alijeruhiwa katika shambulio dhidi ya askari walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha amani Darfur , UNAMID, July 13 ambapo askari saba walinda amani kutoka Tanzania waliuwawa.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini New York Katibu Mkuu amesema askari huyo amefariki jana katika hospitali iitwayo Khartoum. Bwana Ban ametoa salamu zake za rambirambi kwa familia na marafiki waliompoteza askari huyo na kusema ana matarajio kwamba serikali ya Sudan itachukua hatua za haraka kuwafikisha watuhumiwa katika vyombo vya sheria.