Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yasaini mkataba wa udhibiti wa biashara ya silaha, Ban apongeza

Marekani yasaini mkataba wa udhibiti wa biashara ya silaha, Ban apongeza

Idadi ya nchi zilizotia saini mkataba wa kimataifa unaodhibiti biashara ya silaha leo imeongezeka na kufikia zaidi ya nusu ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa. Kufuatia hatua hiyo Katibu Mkuu wa Ban Ki-moon ambaye ndiye mwangalizi wa mkataba huo hutoa pongezi kwa kila nchi inapotia saini lakini kwa hatua ya leo imekuwa na umuhimu zaidi kwa kuwa Marekani nchi inayoongoza kwa kuuza silaha duniani nayo imefanya hivyo.

Amesema ni matumaini yake kuwa kitendo hicho kitachangia jitihada za kupunguza ukosefu wa usalama na machungu wanayopata watu duniani kote huku akitaka mataifa ambayo bado hayajasaini kufanya hivyo.