Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na Rais wa Brazili Bi Dilma Rousseff:

Ban akutana na Rais wa Brazili Bi Dilma Rousseff:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na Rais wa Jamhuri ya Brazil Bi Dilma Rousseff. Ban amemshukuru Rais kwa mchango mkubwa wa Brazili katika kuunga mkono masuala ya viupaumbele vya Umoja wa Mataifa.

Ban amesema mchango mkubwa wa Brazili kufuatia mkutano wa Rio+20 wa maendeleo endelevu ni suala ambalo halitosahaulika, mchango wa taifa hilo kwa Haiti na kazi kubwa ya vikosi vya Brazil kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa Haiti MINUSTAH imepongezwa saana na Umoja wa mataifa. Masuala mengine waliyozungumzia ni hali inayoendelea Mashariki ya Kati pamoja na mgogoro wa Syria.